Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa ECOWAS kukutana Abuja

Wakuu ECOWAS Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa ECOWAS kukutana Abuja

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Voa

Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa jumuia ya uchumi ya mataifa ya Afrika magharibi (ECOWAS) wanakutana katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kuanzia leo Jumatano hadi Ijumaa kujadili mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, jumuiya hiyo imesema.

Siku ya Jumapili, ECOWAS iliiwekea vikwazo Niger na kuonya kuwa inaweza kutumia nguvu huku ikiupa utawala wa kijeshi muda wa wiki moja kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Afisa wa ECOWAS pia aliiambia AFP jana Jumanne kwamba ujumbe wa jumuiya hiyo unaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar utafanya ziara Niger leo Jumatano.

Mapinduzi hayo yamezitia wasiwasi nchi za magharibi zinazojitahidi kudhibiti uasi wa wanamgambo wa kiislamu uliozuka kaskazini mwa Mali mwaka 2012, na kuingia Niger na Burkina Faso miaka mitatu baadaye na sasa unatishia mataifa dhaifu katika Ghuba ya Guinea.

Raia kadhaa, wanajeshi na polisi wameuawa katika eneo hilo lote, wengi katika mauaji ya kikatili, huku watu milioni 2.2 nchini Burkina Faso pekee wakiwa wamehama makazi yao.

Chanzo: Voa