Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakuu wa Majeshi wa EAC wakutana mjini Nairobi

Eac Sudan.jpeg Wakuu wa Majeshi wa EAC wakutana mjini Nairobi

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha kijeshi cha jumuiya ya Afrika Mashariki cha {EAST AFRICA STAND BY FORCE} kitakuwa tayari kukabiliana na hali mbaya ya usalama ambayo inashuhudiwa kwenye mataifa kadhaa ambayo ni wanachama wa jumuiya ya EAC.

Akizungumza katika mkutano wa 32 wa kikosi hicho ulioandaliwa Nairobi ambao pia umehudhuriwa na mkuu wa jeshi la Kenya Jenerali Francis Ogolla amesema kwamba changamoto za kiusalama ambazo zinaikumba eneo hili zimebadilika na tishio la usalama kwa raia lipo hasa katika maeneo ambayo yanakumbwa na mapigano na vile vile tishio la ugaidi.

‘’Mabadiliko haya yanatulazimu kujirekebisha vilivyo na kubuni mbinu za kisasa katika ari yetu ya kudhibiti tishio lililopo. Wakati huu tunajikuta katikati hali ngumu ya kisiasa na kiusalama kwenye kanda hii huku baadhi ya tishio za kiusalama zikivuka mipaka ya mataifa wanachama ambazo zinatuhitaji kukabiliana nayo kwa Pamoja,’’ alisema Jenerali Ogolla.

Mkurugenzi wa kikosi hicho cha EASF Brigedia Paul Kahuria Njema amesema kwamba, kutokana na hali ilivyo katika eneo hili, kuna haja ya mataifa husika kushirikiana katika masuala ya ujasusi, ulinzi na kutoa huduma muhimu za kuhakikisha kwamba hali ya usalama inadhibitiwa na kuwafaa raia ambao wanahangaika katika baadhi ya mataifa ambayo yanakumbwa na mapigano na vita.

‘’Ili kuwa na uwezo wa kukabiliana vyema na tishio lililopo katika eneo hili, tunapendekeza kufanyia mabadiliko mfumo wa sera uliopo pamoja na stakabadhi za kutekeleza majukumu ili kikosi cha EASF kiweze kukabiliana, kudhibiti na kuzuia tishio la hali mbaya ya usalama,’’ alisema Brigedia Kahuria.

Wakuu wa kikosi cha EASF wamesema kwamba kiko tayari kutekeleza majukumu kadhaa katika baadhi ya mataifa ya eneo hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live