Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakuu wa AU kukutana nchini Ethiopia kwa mkutano wa kila mwaka

AU AU Umoja Wa Afrika.png Wakuu wa AU kukutana nchini Ethiopia kwa mkutano wa kila mwaka

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwishoni mwa juma, viongozi wa umoja wa Afrika watakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwa mkutano wa kila mwaka ambapo ajenda kuhusu Amani na usalama wa kikanda inatarajiwa kuwa kipaumbele cha majadiliano yao.

Mkutano huu unaenda kufanyika wakati ambapo AU inanyooshewa kidole kwa kushindwa kutatua mizozo inayokabili bara hilo na hasa ongezeko la mapinduzi ya kijeshi katika eneo la Afrika Magharibi.

Hata hivyo, wadadisi wa mambo wanahoji ukimya wa AU kwa mwenyeji wa mkutano huo nchi ya Ethiopia, ambayo kwa muda imeshuhudia vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye eneo la Tigray, na mauaji yanayoripotiwa hivi sasa huko Amhara.

Mbali na mizozo ya ndani, uhusiano wa Addis Ababa na nchi jirani ya Somalia, umeingia baridi baada ya serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza makubaliano ya bandari kati yake na eneo lililotangaza kujitenga la Somaliland, haya yote AU ikishindwa kuikemea ipasavyo Ethiopia.

Maswali kuhusu ukimya wa AU kwa vitendo vya Ethiopia, yaliongezeka zaidi juma hili wakati mkuu wa kamisheni ya umoja huo, Moussa Fakhi Mahamati, akiutaja mizozo ya Sudan na Chad, bila hata sehemu moja kuizungumzia Ethiopia.

Mbali na mzozo wa Ethiopia, maswali mengine yaliyobaki ni je, viongozi hao wataweza kutoa suluhu ya mzozo unaoendelea kwenye nchi za Mali, Burkina Faso, Niger, Gabon na Guinea?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live