Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima 30 wauawa katika shambulio la wabeba silaha Nigeria

Wakimbizi Wa Ndani Watekwa Nyara Nchini Nigeria Wakulima 30 wauawa katika shambulio la wabeba silaha Nigeria

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa akali wakulima 30 wameuawa katika shambulizi la genge la wabeba silaha katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Msemaji wa Kamandi ya Polisi ya Zamfara, Yazid Abubakar amesema katika taarifa kuwa, kundi hilo la magaidi lilifanya shambulio hilo la umwagaji damu jana Ijumaa katika maeneo ya Maradun na Tsafe.

Amesema mwanachuoni maarufu wa Kiislamu, Mallam Makwashi Maradun Mai Jan-Baki ni miongoni mwa watu zaidi ya 10 waliouawa katika shambulio hilo katika eneo la Maradun.

Shirika la habari la Iran Press limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, watoto wawili wa kiongozi huyo mashuhuri wa kidini aliyeuawa, hawajulikani walipo kufuatia hujuma hiyo.

Habari zaidi zinasema, watu zaidi ya 20 wameuawa katika shambulizi la pili la wabeba silaha hao lililolenga kijiji cha Bilbis katika eneo la Tsafe jimboni Zamfara.

Magaidi wabeba silaha jimboni Zamfara Licha ya kwamba jeshi la Nigeria linaendelea kupiga kambi katika jimbo hilo tokea mwaka 2016 kwa ajili ya kuimarisha usalama, lakini bado makundi ya wabeba silaha ambayo yamekuwa yakifanya wizi na magendo, yanaendelea kufanya jinai na uhalifu.

Mamia ya wanavijiji wameuawa katika mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi hayo ya wabeba silaha katika jimbo hilo la Zamfara, la kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live