Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakongo wapinga uwepo wa jeshi la Afrika Mashariki

Wakongo Wapinga Uwepo Wa Jeshi La Afrika Mashariki Wakongo wapinga uwepo wa jeshi la Afrika Mashariki

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Muungano wa vyama vya kiraia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umefanya maandamano mjini Goma ukitaka kikosi cha pamoja cha Afrika Mashariki kuondoka mashariki mwa nchi hiyo kutokana na kushindwa kukabiliana na waasi wa M23.

Mwezi Novemba mwaka jana, Kenya, Burundi, Uganda na Sudan Kusini zilituma wanajeshi wake DR Congo, chini ya bendera ya Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF), kujaribu kulipokonya silaha kundi hilo la waasi na kuleta amani.

M23 imeendelea kushikilia baadhi ya miji na vijiji katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Watu saba waliuawa mapema mwezi huu katika eneo hilo.Wiki iliyopita, msemaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Patrick Muyaya aliithibitishia BBC kwamba serikali yake haitawapatia kandarasi mpya wanajeshi wa EACRF.

Alisema kuwa wanajeshi wa Kongo watafanya kazi nzuri zaidi akiongeza kuwa EACRF inapaswa kuondoka mwishoni mwa agizo hilo mwezi Desemba.

Katika taarifa ya hivi karibuni Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema vikosi vyake vimejitolea kufanya kazi kwa karibu na serikali kuwezesha kurejea salama kwa wakimbizi wa ndani kwenye makazi yao na kuimarisha ulinzi wa raia kwa ujumla.

Goma pia imeshuhudia maandamano mabaya dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Zaidi ya watu milioni 6.2 wamelazimika kuondoka makwao mashariki mwa nchi hiyo na wanaishi kwingine nchini DR Congo, na wengine milioni moja wametafuta hifadhi zaidi ndani ya Afrika, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Chanzo: Bbc