Asilimia 95 ya Wakimbizi na waomba hifadhi wa nchi ya Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu Wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamegoma kurejea nchini kwao, kwa kile wanachodai bado hali ya amani hairidhishi
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu Siasa Manjenje amesema hayo wakati wa mkutano wa viongozi wa Idara ya wakimbizi kutoka Tanzania na Burundi na kamati za ulinzi na usalama kutembelea kambini hapo, huku wakimbizi mwenyewe akieleza sababu kuwa, hawaamini hali ya usalama kuimalika nchini mwao.
Kwa upande wake mkurugenzi idara ya huduma kwa wakimbizi Nchini, Sudi Mwakibasi amewataka wakimbizi kuendelea kulejea kwa kasi na kulingana na Warundi wenzao katika Kujenga Taifa hilo.
Aidha mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye na Naibu waziri wa mambo ya ndani nchini Burundi Nibona Bonansize wamewahakikishia wakimbizo hao Nchi ya Burundi kuwa Shwari na kwamba hawana budi kuendelea kuishi kama wakimbizi mbali wakajenge Nchi yao.