Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi bado kupata mahitaji Tigray

0fdf9514f0a173910cff621437ed0e71 Wakimbizi bado kupata mahitaji Tigray

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIBU Msemaji wa Katibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema watu wengi katika Mkoa wa Tigray hawajapata msaada wowote kwa zaidi ya wiki sita tangu kuanza kwa mapigano katika mkoa huo.

Alisema Shirika la Uhamiaji la Kimataifa lilipeleka msaada kwenye maeneo ya mpaka ya Tigray wakati Shirika la Chakula Duniani (WFP) nalo lilipeleka chakula kwenye kambi huko Tigray.

“Tunaendelea kutoa mwito kwa ufikiaji wa haraka na bila mipaka kwa maeneo yote ambayo watu wameathiriwa na mapigano. Wenzetu wa misaada ya kibinadamu walituambia kwamba licha ya umeme na mawasiliano ya simu vinafanya kazi kwa vipindi katika Mji Mkuu wa Tigray, Makelle, watu katika maeneo mengine mengi ya mkoa huo bado hawana chakula, maji, fedha, umeme na mawasiliano ya simu,”alisema Haq.

Alisema wakimbizi kati ya 200 hadi 300 wanaendelea kuwasili kila siku katika nchi jirani ya Sudan. Mapigano hayo yalizuka mwezi uliopita kati ya waasi wa Tigray na serikali ya shirikisho na kusababisha raia kukosa mahitaji ya msingi, wengi kukimbia makazi yao huku kambi za wakimbizi zikikosa mahitaji ya msingi.

Chanzo: habarileo.co.tz