Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi DRC walia na mengi!

Wakimbizi Drc Drc.jpeg Wakimbizi DRC walia na mengi!

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya raia wanaokimbia mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 huko wilayani Masisi,wahangaika kwenye mji mdogo wa Sake ulio umbali wa kilometa 25 kutoka Goma.Wakimbizi hao hawana sehemu za malazi wala vyakula.

Baadhi ya raia hao, ni watoto na wanawake wanaokimbia mapigano yanayoendelea hadi sasa wilayani Masisi kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23.

Wakiwa na mizigo yao hususan magodoro kando na barabara za mji huu wa Sake wanazungumzia hali wanayoipitia.

“Tuliwasili hapa kwa sababu ya mapigno, na hivi tupo nje hatuna mahali pa kulala,hatuna hata chakula na hiyo imekuwa ni tatizo kubwa kwetu .walisema baadhi ya wakimbizi hao.

Wakimbizi hao wamekuwa na uhitajii mkubwa wa msaada wa dharura. Justin Tukuzwe, kijana mkimbizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live