Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi 600 warudi nyumbani

1da7bd27c5015fba38f99dbc98ce67df Wakimbizi 600 warudi nyumbani

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKIMBIZI zaidi ya 600 wa Burundi waliokuwa wakiishi nchini Uganda kwa zaidi ya miaka 10 hatimaye wamerejea nyumbani kwa hiyari yao baada ya kuhakikishiwa hali ya usalama na utulivu nchini.

Kurejea kwa wakimbizi hao kumefanikishwa na ushirikiano mkubwa kati ya serikali ya Burundi na ya Uganda kwa usimamizi wa karibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR).

Kundi la kwanza la wakimbizi hao wapatao 61 walisafirishwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uganda wakitokea Entebbe na kwenda Bujumbura nchini Burundi.

Kabla ya wakimbizi hao kusafirishwa, serikali ya Uganda kwa kushirikiana na UNHCR ilihakikisha taratibu zote za kiafya zimezingatiwa pamoja na kuchukua vipimo vya maambukizi ya virusi vya corona na wakimbizi wote kukutwa wakiwa hawana maambukizi hayo.

Wakimbizi hao walisindikizwa na Godfrey Byaruhanga na Arthur Mugarura kutoka katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Dancun Mato kutoka UNHRC.

Chanzo: habarileo.co.tz