Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi 500 warejea Burundi kutoka Rwanda

443453a950bdf2193a1465115c5848ea Wakimbizi 500 warejea Burundi kutoka Rwanda

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKIMBIZI wa Burundi takribani 500 waliokuwa wakiishi nchini Rwanda, wamerejea nchini mwao, likiwa ni kundi la kwanza tangu walipokimbia nchi yao miaka mitano iliyopita.

Wizara ya Usimamizi wa Majanga Rwanda ilieleza kuwa, kundi la wakimbizi 500 mpaka 600 waliwasili nchini humo juzi baada ya kuondoka Rwanda Alhamisi iliyopita.

Taarifa ya wizara hiyo ilieleza kuwa, wakimbizi hao waliondoka katika kambi ya Mahama wilaya ya Krehe nchini Rwabda kupitia mpaka wa Nemba, wilaya ya Bugesera.

Kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao kunatokana na maombi yaliyotolewa mwezi uliopita ya wakimbizi wa Burundi zaidi ya 330 waliopo katika kambi ya Mahama kutaka kurejea nchini mwao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Dk Vincent Biruta, alisema hakuna mkimbizi aliyezuiliwa kurejea nyumbani kama ilivyodaiwa awali.

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), zinaonesha kuwa, Rwanda ina wakimbizi 77,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na 71,000 kutoka Burundi, huku kambi ya Mahama pekee ikiwa na wakimbizi 60,000.

Chanzo: habarileo.co.tz