Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi 4,000 warejea nchini

B494663a31806d5053fabc79dd307030 Wakimbizi 4,000 warejea Sudan

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKIMBIZI zaidi ya 4,000 wamerejea nchini hadi Desemba mwaka jana kutoka nchi jirani.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Tume ya Usaidizi na Ukarabati ya Sudan Kusini (RRC) ameeleza kuwa, wakimbizi 4,036 wamethibitishwa kurejea nchini idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na 7,981 waliorejea Novemba, mwaka jana.

Alisema asilimia 61 ya wakimbizi waliorejea wametoka Sudan, wakati asilimia 23 wakitokea Ethiopia na asilimia 15 wametokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Uganda na Kenya.

Alisema wengi wamerejea katika majimbo ya Unity asilimia 61, Upper Nile asilimia 16 na Jonglei asilimia 11.

Wakimbizi hao waliorejea kwa wingi kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana kwa kutumia mipaka ya Sudan na Ethiopia.

Hata hivyo, mpaka wa Nimule kati ya Sudan Kusini na Uganda ni kati ya iliyoingiza wakimbizi wengi.

Taarifa ya UNHCR inaeleza kuna wakimbizi wengine 2,813 wa Sudan Kusini wapo katika harakati za kuvuka mpaka wa Uganda kurejea nchini humo wakati wakisubiri uhakiki wa maeneo watayapofikia.

Wakimbizi wanaorejea, waliieleza UNHCR na RRC kuwa njiani wamekumbana na matukio ya ulaghai, kukamatwa, na unyanyasaji na mamlaka katika vituo vya mipaka ya Nadapal na Nimule ambayo ni kati ya Kenya na Uganda.

Chanzo: habarileo.co.tz