Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakimbizi 20 wauawa katika mkanyagano Niger

Wakimbizi 20 wauawa katika mkanyagano Niger

Wed, 19 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Niamey, Niger. Zaidi ya watu 20 wameuawa katika mkanyagano kwenye kambi ya wakimbizi iliyopo katika Mkoa wa Diffa, Niger.

Taarifa ya serikali ya Niger alisema wakimbizi hao walikufa baada ya kukanyagana wakati wa mgao wa chakula na mahitaji mengine.

Gavana wa Mkoa wa Diffa, Issa Lamine alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Jumanne Februari 18.

Gavana huyo alisema waliopoteza maisha ni pamoja na wanawake 15 na watoto watano wanaoishi katika kambi hiyo.

Gavana Lamine alisema watu wengine 16 walijeruhiwa katika mtafaruku huo na kupatiwa matibabu.

Kwa zaidi ya muongo mmoja sasa kundi la Boko Haram lililopo Kaskazini mwa Nigeria limekuwa likiendesha mapigano yanayosababisha mauaji huku wengi wakikimbia makazi yao na kuingia nchini Niger ili kupata hifadhi.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz