Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili mashuhuri adai maisha yake yamo hatarini baada ya kumkosoa Uhuru kortini

A3675b02c3e8a709 Wakili mashuhuri adai maisha yake yamo hatarini baada ya kumkosoa Uhuru kortini

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wanaume wawili waliokuwa wanadai kuwa makacheoro wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) walivamia ofisi ya John Khaminwa JumamosiHaya yanajiri siku moja baada ya kutoa kauli yake dhidi ya kesi ya rufaa ya Mpango wa Maridhiano(BBI) katika Mahakama ya Rufaa Wakili huyo alitaja kisa hicho kama cha kumtishia maisha kwani kesi hiyo ya rufaa ilikuwa imewavuta watu tofauti kote ulimwenguni

Wakili mashuhuri John Khaminwa sasa anadai kuwa maisha yake yamo hatarini baada ya kauli yake katika Mahakama ya Rufaa dhidi ya kesi ya Mpango wa Maridhiano.

Katika kikao cha Ijumaa, Julai 2, wakili huyo aliambia jopo la majaji saba wanaosikiza kesi hiyo kutupilia mbali rufaa ya Rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza Jumamosi, Julai 3, Khaminwa alisema kuwa mawakili wanaopinga rufaa ya BBI wanatishwa na kunyanyaswa.

Hii ni baada ya wanaume wawili waliokuwa wanadai kuwa makacheoro wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) walivamia ofisi ya John Khaminwa Jumamosi.

Wakili huyo alitaja kisa hicho kama cha kumtishia maisha kwani kesi hiyo ya rufaa ilikuwa imewavuta watu tofauti kote ulimwenguni.

Isitoshe, Khaminwa alimtaka Inspekta Jenerali wa Polisi kuhakikisa kuwa mawakili walioshiriki katika kesi ya BBI wanapewa usalama.

EACC yakanusha kuvamia KhaminwaKwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa EACC, Twalib Mbarak alikanusha madai kuwa makachero wa tume hiyo ndio walivamia ofisi za Khaminwa.

"EACC ingelipenda kufahamisha umma kuwa haikufanya operesheni yeyote jan ana ripoti zinazodai kuwa EACC ilivamia afisi za wakili John Khaminwa si za kweli," ilisema EACC.

Khaminiwa akiwakilisha Tume ya Kutetea Haki ya Binadamu Nchini na Kituo Cha Sheria alihoji kuwa Rais Uhuru huwa hatii maagizo ya mahakama, na hukiuka mara kwa mara Katiba.

''Bwana wangu, kwa unyenyekevu ningelipenda kusema wakati unafika mbele ya mahaka ma hautakani kuwadharau majaji, na tena wakati huo huo unatarajia kufika mbele ya jaji huyo akupe amri,''

"Wakati una rais ambaye haheshimu korti, wakati una rais ambaye anadharau majaji mbele ya umma, korti hii inatakiwa kusimama kidete na kusema haitamsikiza hatuwezi kupa amri kabisa," Khaminwa alisema.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke