Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili azua gumzo mitaani kwa kumfulia mkewe nguo

Wakili Azua Gumzo Mitaani Kwa Kumfulia Mkewe Nguo.png Wakili azua gumzo mitaani kwa kumfulia mkewe nguo

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wakili maarufu amegusa mioyo ya wengi baada ya kumfulia mkewe nguo na kufanya kazi zingine za nyumbani.

Peter Wanyama alisema kuwa yeye hufanya hivyo wakati akiwa nyumbani na wanawe. Aliongeza kuwa ni jambo ambalo amekuwa akifanya wakati ambapo aidha mfanyakazi au mkewe hawako nyumbani.

“Mke wangu anaposhindwa kufanya kazi za nyumbani, na msaidizi wa nyumbani hayupo kwa sababu yoyote ile, mimi husaidia kazi za nyumbani kwa sababu mimi ndiye kiongozi wa nyumbani,” alisema.

Wakati huu, Wanyama alikuwa na sababu kubwa zaidi ya kusaidia kazi za nyumbani nyumbani,baada ya mkewe kufanyiwa upasuaji wakati akijifungua.

Kwa bahati mbaya wakili Peter na mkewe walimpoteza mwanao,jambo ambalo lilipelekea mkewe kuzama kwenye lindi la mawazo.

"Kama wakati huu mke wangu alikuwa amefanyiwa upasuaji, lakini cha kusikitisha ni kwamba, tulipoteza mtoto wetu. Tulimzika mtoto wetu wiki mbili zilizopita. Kusaidia nyumbani ni kuonyesha uongozi kwa vitendo," alisema.

Jamii kwa kawaida humchukia mwanamume anayefanya kazi za nyumbani kama mtu ambaye anadhalilishwa kiheshima, lakini Wanyama alisema kuwa hilo halimuathiri.

Wanyama aliwasauri wanaume wenzake akisema ni vyema kubadili dhana hiyo ambayo imepitwa na wakati na kuwa msitari wa mbele kwa maswala yanayohusu familia kwa vitendo.

Alisema kuwa yeye husaidia kufanya shughuli zote zikiwemo kupika na hata kuenda sokoni kutafuta vyakula.

"Hiyo ni dhana potofu; lazima tubadili fikra hizo. Lazima tutoe uongozi wa kimkakati katika jamii. Mbali na kufua, pia ninapika na kwenda sokoni; najua jinsi ya kununua mboga bora sokoni," alisema.

Alipoweka picha yake akifua nguo kwenye Facebook, watumiaji wa mtandao walikuwa na mengi ya kusema na hapa chini ni baadhi ya maoni.

"Love this! Asante kwa kusaidia na kumruhusu mkeo kipenzi apumzike anapopata nafuu. Mungu aibariki kazi ya mikono yako,"aliandika mtumiaji mmoja wa mtandao.

Chanzo: Radio Jambo