Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili apigwa faini kwa kutaka kusitisha kuapishwa kwa Tinubu

Wakili Apigwa Faini Kwa Kutaka Kusitisha Kuapishwa Kwa Tinubu Wakili apigwa faini kwa kutaka kusitisha kuapishwa kwa Tinubu

Fri, 26 May 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama nchini Nigeria imemtoza faini aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi wa 2019 kwa kuwasilisha kesi ya kusitisha kuapishwa kwa Rais mteule Bola Tinubu tarehe 29 Mei.

Mahakama iliamuru Ambrose Owuru, wakili, kulipa $87,000 (£80,000) kwa kufuata kesi ya "ajabu" na "isiyo na maana". Bw Owuru, ambaye aligombea na kushindwa katika uchaguzi wa urais wa 2019, alikuwa ameitaka mahakama iamuru aapishwe kama rais badala ya Bw Tinubu.

Wakili huyo, ambaye hakushiriki uchaguzi wa urais wa 2023, alidai alishinda uchaguzi wa urais wa 2019 lakini alinyimwa ushindi wake isivyo haki.

Ikitupilia mbali kesi hiyo mnamo Oktoba 2019, Mahakama ya Juu ilieleza kuwa ni matumizi mabaya ya mchakato wa mahakama.

Baada ya Bw Tinubu kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa 2023, Bw Owuru aliwasilisha kesi nyingine kutokana na ukweli wa kesi yake ya 2019.

Jopo la watu watatu wa Mahakama ya Rufaa katika mji mkuu Abuja walitupilia mbali kesi hiyo katika uamuzi ulioafikiwa siku ya Alhamisi.

Chanzo: Bbc