Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wavuta pumzi huku bei ya umeme ikishuka

Wakenya Wavuta Pumzi Huku Bei Ya Umeme Ikishuka Wakenya wavuta pumzi huku bei ya umeme ikishuka

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Watumiaji wa Umeme wanaweza kupata nafuu huku bei ikitarajiwa kupungua kuanzia saa sita usiku.

Kulingana na Wizara ya Nishati, bei za umeme kwa aina zote za watumiaji zitapungua kwa Ksh.3.44 kwa kila uniti.

Katibu Mkuu wa Kawi Alex Wachira amehusisha marekebisho hayo na kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji wa fedha za kigeni.

"Mabadiliko ya kiwango cha ubadilishaji wa fedha za kigeni yalipungua kutoka Ksh.6.46 kwa kilowati hadi Ksh.3.22 kwa kilowati kutokana na kupungua kwa jumla ya malipo ya ubadilishaji wa fedha za kigeni yaliyofanywa Januari," alisema Jumatano.

PS Wachira pia alihusisha mabadiliko ya bei na punguzo la chini la gharama ya Nishati ya Mafuta ambayo ilishuka kwa senti 19.

Watumiaji wa malipo ya awali wataona mabadiliko hayo kuanzia saa sita usiku, huku wanaolipa baada ya kutumia watalipa kiasi kidogo mwishoni mwa Februari.

Chanzo: Bbc