Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya watahadharishwa ulaji nyama ya nguruwe na kuku!

Wakenya Watahadharishwa Ulaji Nyama Ya Nguruwe Na Kuku! Wakenya watahadharishwa ulaji nyama ya nguruwe na kuku!

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Kenya Kenya (KEMRI), kwa ushirikiano na Shirika la Kulinda Wanyama duniani, na Kituo cha Utafiti wa Mikrobiolojia, imewatahadharisha Wakenya kuhusu nyama ya nguruwe na kuku inayouzwa katika maduka makubwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti hao, nyama inayouzwa kwenye maduka hayo ilikuwa na viwango vya bakteria walio sugu kwa dawa hivyo kuwa na madhara kwa walaji.

Zaidi ya mwaka mmoja, sampuli zilikusanywa kutoka maduka makubwa katika miji mitano, ambayo ni Nairobi, Kisumu, Nakuru, Nanyuki, na Eldoret, na majaribio yalifanywa katika taasisi ya serikali.

Utafiti huo ulibaini kuwa hali hii inaweza kuongezeka na kuwa janga la kimya kwa kuwa watu ambao wameathirika na ugonjwa huo wanaugua lakini dawa zilizopo haziwezi kuwatibu. Bakteria sugu kwa dawa.

Zaidi ya hapo, kulingana na Victor Yamo, mwanasayansi anayeshughulikia Ulinzi wa Wanyama Ulimwenguni, shida huanzia shambani wakati mkulima anaweka nguruwe na kuku kwenye mazingira machafu.

Amesema ni muhimu kutekeleza viwango vya juu vya usafi wa chakula na usafi wa mazingira wakati wote wa usambazaji, haswa wakati wa kuchinja na ufungaji, ili kuzuia kuingizwa kwa bakteria kwenye chakula na kuenea kwa vimelea vya chakula.

Alilinganisha hali hiyo na janga, ambapo maisha milioni tatu yalipotea. Yamo amesema ikiwa hali hiyo itaendelea, watu wasiopungua milioni 10 wanaweza kufariki dunian kila mwaka.

Mnamo 2019, mwandishi wa habari Dennis Okari alifichua jinsi maafisa wa maduka makubwa wasio waaminifu wanavyotumia kemikali kuongeza muda wa matumizi ya bidhaa za nyama.

Chanzo: Bbc