Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wapanda miti kuwakumbuka waliofariki katika wa mafuriko

Wakenya Wapanda Miti Kuwakumbuka Waliofariki Katika Wa Mafuriko Wakenya wapanda miti kuwakumbuka waliofariki katika wa mafuriko

Fri, 10 May 2024 Chanzo: Bbc

Maafisa wa Kenya wanaongoza zoezi la upandaji miti kote nchini kama sehemu ya siku ya kitaifa ya maombolezo ya waliofariki katika mafuriko yaliyosababisha vifo vya hivi majuzi.

Rais William Ruto ametoa wito kwa wakenya kujumuika kupanda miti akisema mafuriko na ukame ni masuala ya mazingira.

Akizungumza katika hafla ya upandaji miti katikati mwa Kenya siku ya Ijumaa, alimtaka kila Mkenya kupanda angalau miti 50 ili kutimiza lengo la siku hiyo la kupanda miti milioni 200.

Maafisa wengine wa serikali, wakiwemo mawaziri, wanaongoza zoezi sawa na hilo kote nchini.

Mafuriko katika wiki za hivi majuzi yamesababisha vifo vya takriban watu 230 na kuwafanya zaidi ya robo milioni kuyahama makazi yao.

Serikali ilitangaza Ijumaa kuwa sikukuu ya umma kwa Wakenya kupanda miti na kuwakumbuka waliofariki katika mkasa huo.

Chanzo: Bbc