Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wanatengeneza pombe haramu Uarabuni -Waziri

Wakenya Wanatengeneza Pombe Haramu Uarabuni  Waziri Wakenya wanatengeneza pombe haramu Uarabuni -Waziri

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua amesema kuna raia wa ughaibuni wanaotengeneza pombe haramu katika nchi za Kiarabu ambako hairuhusiwi.

"Inasikitisha sana...kuna Wakenya ughaibuni wanatengeneza pombe za kienyeji 'chang'aa', na kuuza kwa Waafrika wengine kinyume na sheria za nchi za Kiislamu," alisema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ndani, Citizen TV.

Alisema Wakenya wanaofanya shughuli haramu wanahujumu jitihada za serikali katika kushughulikia masuala ya ustawi wa raia wake nje ya nchi.

Alikuwa akijibu wasiwasi kuhusu baadhi ya Wakenya wanaokabiliwa na matatizo ikiwa ni pamoja na ripoti za unyanyasaji wa watu wanaofanya kazi Mashariki ya Kati.

Alisema serikali inafanya kila iwezalo kuboresha ustawi wa Wakenya huko.

Alisema aliona hali si "mbaya jinsi inavyosikika" alipotembelea Saudi Arabia mara tu baada ya kuteuliwa kuwa waziri.

"Tatizo ni kwamba baadhi ya Wakenya hujihusisha na vitendo haramu na uhalifu wanapoenda huko," alisema.

Chanzo: Bbc