Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wakasirishwa na ushuru mpya kwa wasafiri

Wakenya Wakasirishwa Na Ushuru Mpya Kwa Wasafiri Wakenya wakasirishwa na ushuru mpya kwa wasafiri

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Wakenya wanapinga agizo la mamlaka ya mapato linalotaka kutoza ushuru bidhaa za kibinafsi au za nyumbani zenye thamani ya $500 (£400) na zaidi kutokana na watalii wanaozuru na raia wanaorejea nchini.

Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) inasema bidhaa zote ziwe mpya au za mtumba za thamani hiyo zitatozwa ushuru.

Maagizo hayo yamezua taharuki kwa wananchi huku Wakenya wengi wakisema kuwa hatua hiyo itawatia hofu watalii.

Baadhi ya wabunge walisema baadhi ya maafisa wa KRA wamekuwa wakichukua fursa ya agizo hilo kuwasumbua watalii, hali inayoipa nchi sifa mbaya.

Waziri wa Utalii Alfred Mutua alitaja hatua hiyo ya KRA kuwa mojawapo ya sababu ya idadi ya watalii wanaozuru nchini kupungua.

“Wewe nenda Rwanda, hawakusumbui. Je, Rwanda haitoi kodi? Unaenda Afrika Kusini, na hawakusumbui. Huko Dubai, hawakunyanyasi. Kwa hivyo, kwa nini wageni wetu wanakabiliwa na changamoto kama hizi nchini Kenya? Na tunashangaa kwa nini watu hawaji Kenya,” Bw Mutua alisema.

Ni hatua ya hivi karibuni zaidi katika msururu wa ushuru mpya ulioanzishwa na serikali ya Rais William Ruto, ukilaumiwa kwa kuzorota kwa gharama ya maisha nchini.

Hii ni licha ya kwamba Bw Ruto alishinda uchaguzi mwaka jana kwa ahadi ya kupunguza matatizo ya kiuchumi.

Chanzo: Bbc