Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wakasirishwa na ongezeko la tozo

Kenya: Ruto Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mawaziri Wakenya wakasirishwa na ongezeko la tozo

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Wakenya wakasirishwa na ongezeko la tozo katika baadhi ya huduma za serikali Wakenya wamekasirishwa na ongezeko la tozo lililofanywa na serikali kupitia Idara ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia, katika baadhi ya huduma zake ikiwemo hati ya kusafiria, kitambulisho, kibali cha kazi, maombi ya cheti cha kuzaliwa na kifo na huduma nyinginezo.

Katika notisi maalum ya gazeti la serikali ya Novemba 7, 2023, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani Prof. Kithure Kindiki alitangaza mabadiliko hayo ya tozo.

Mfano ombi la kawaida la pasipoti ya kurasa 34 imepanda hadi Ksh.7,500 kutoka Ksh.4,500.

Pasipoti ya kawaida ya kurasa 50 sasa itagharimu waombaji Ksh.9,500 kutoka Ksh.6,000 huku ada ya maombi ya pasipoti ya kawaida ya kurasa 66 ikipanda kwa Ksh.5,000 hadi Ksh.12,500.

Ada ya pasipoti ya kidiplomasia ya kurasa 50 imeongezeka maradufu hadi Ksh.15,000 kutoka Ksh.7,500 ilhali tozo ya pasipoti ya huduma ya kurasa 32 ikisalia kuwa Ksh.3,000.

Kubadilisha pasipoti iliyopotea kutagharimu Ksh.20,000, ongezeko la Ksh.8,000 kutoka ada ya awali huku kubadilisha pasi halali iliyokatwa kutagharimu Ksh.20,000 kutoka Ksh.10,000.

Bei ya vibali vya muda, vyeti vya utambulisho na hati za usafiri wa dharura itasalia kuwa vilevile Ksh.300, Ksh.3,000 na USD 20 (takriban Ksh.3031 kulingana na kiwango cha ubadilishaji cha sasa) mtawalia.

Zaidi ya hayo, hati za kusafiria za wakimbizi zitatolewa bila gharama yoyote.

Waombaji wa vitambulisho kwa mara ya kwanza watalipa Ksh.1,000 ili kupata hati ambazo zilitolewa awali bila gharama yoyote.

Ubadilishaji wa vitambulisho vilivyopotea utahitaji malipo ya Ksh.1,000, kuashiria ongezeko mara kumi kutoka Ksh.100 .

Hata hivyo kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Wakenya walionyesha hisia tofauti kufuatia hatua hiyo.

Chanzo: Bbc