Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya waishitaki Uingereza madai unyanyasaji wa kikoloni

Ukoloni Kenya Kesi Wakenya waishitaki Uingereza madai unyanyasaji wa kikoloni

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Wakenya wamewasilisha kesi dhidi ya serikali ya Uingereza katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) kwa madai ya unyanyasaji wa kikoloni.

Hizi ni pamoja na madai ya wizi wa ardhi, ambayo bado inatumiwa na makampuni ya chai.

Koo hizo zinasema madai ya kutoshiriki kwa Uingereza kutafuta suluhu kumekiuka Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu.

Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza imeiambia BBC kwamba ‘’haikuwa sawa kutoa maoni kuhusu kesi za kisheria’’.

Wawakilishi wa Talai na Kipsigis, ambao wanatoka kaunti ya Kericho, wanasema walijaribu kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss mnamo Mei 2022 lakini wakakataliwa.

Ukoo wa Talai unasema wanachama wake walifurushwa kwa nguvu kutoka kwa ardhi yenye rutuba katika nyanda za juu za Bonde la Ufa kwa ajili ya mashamba ya chai.

Watalai waliongoza upinzani dhidi ya makazi ya Uropa.

Ili kukomesha hilo, kila mwanaukoo aliwekwa kizuizini katika bonde lililojaa mbung'o na mbu karibu na Ziwa Victoria la sasa.

Hali za huko zimerekodiwa kuwa mbaya kiasi kwamba wengi wao walikufa na wanawake kukumbana na kuharibika kwa mimba.

Pia walipoteza mifugo yao kwa wingi.

Kenya ilipopata uhuru mwaka wa 1963, walionusurika waliondoka kizuizini na kurudi katika ardhi waliyoiona kuwa ya mababu zao.

Lakini hawakuipata tena.

Wanasema wameishi kando ya mashamba ya chai kama maskwota tangu wakati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live