Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya kulipa ada katika vituo vya Huduma CS

Wakenya Kulipa Ada Katika Vituo Vya Huduma CS.png Wakenya kulipa ada katika vituo vya Huduma CS

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Waziri wa Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji Moses Kuria amesema kuwa huenda wakenya wakaanza kulipia ada katika Majengo ya Hudama Centres, hili kuwezesha vituo 52 vya Huduma kote nchini.

Akifafanua zaidi, Kuria alisema kupitia ada hizo, Huduma centers zitaweza kujipatia mapato ambayo yatapunguza shinikizo kwa hazina.

"Kwa muda mrefu (Wakenya) mmekuwa mkifurahia huduma hizi bila kulipa, Sasa hakuna tena cha bure, mnapaswa kulipia,Tutaanzisha ada ya huduma ya serikali kusaidia biashara yetu ya mtandaoni kwa sababu Huduma Center itakuwa,uti wa mgongo wa biashara ya mtandaoni,” alisema.

Kuria alikuwa akizungumza wakati wa uchukuaji rasmi wa Idara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji kutoka kwa Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa.

Waziri huyo alikuwa amehudumu katika idara ya Biashara kwa muda wa miezi 11 hadi mabadiliko ya hivi majuzi ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais William Ruto ambayo yalimfanya ahamishwe hadi wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji.

Baadhi ya huduma zitakazogharamiwa katika vituo vya Huduma ni pamoja na kusasisha leseni za udereva, nakala za vitambulisho vya kitaifa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Nyingine ni pamoja na usajili na madai ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), HELB – Maombi na Marejesho ya Mikopo ya Wanafunzi, Usajili wa Vikundi vya Ustawi, utoaji wa muhtasari wa polisi, kibali cha biashara moja na tathmini ya ushuru wa stempu miongoni mwa mengine.

Mpango wa Huduma Kenya uliundwa ili kuwezesha utoaji wa anuwai ya huduma za serikali katika kitengo kimoja kinachoitwa Huduma Centers.

Kituo cha kwanza cha Huduma Nairobi kilizinduliwa mwaka wa 2013 na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta pamoja na aliyekuwa Naibu wake wakati huo ambaye sasa ndio Rais wa Kenya William Ruto katika Jengo la Teleposta jijini Nairobi.

Chanzo: Radio Jambo