Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya kukinukisha Mt Meru Marathon

MERU Wakenya kukinukisha Mt Meru Marathon

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By BERTHA ISMAILArusha. ZAIDI ya wanariadha 2000 wanatarajia kushiriki mbio za Mount Meru Marathon 2020 huku Wakenya wakipewa nafasi kubwa ya kukinukisha kwenye mbio hiyo sambamba na wenzao wa Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania.

Mbio hizo zinazofanyika kila mwaka zimepangwa kufanyika Septemba 27 na tofauti na miaka iliyopita Wakenya wamethibitisha kuzishiriki na kuwafanya waandaaji wake kuvutiwa na hatua hiyo, kwani nchi hiyo ilikuwa kwenye karantini ya janga la corona na kuleta wasiwasi wa ushiriki wao.

Mkurugenzi mpya wa mbio hizo Mercy Ntabago amesema msimu huu mbio zao zinazolenga kuhamasisha utalii wa ndani, watatoa pia fursa kwa washindi kutembelea baadhi ya vivutio vya utalii zilizopo mkoani Arusha.

Mercy amesema wameshapeleka barua za ualiko kwa nchi mbali mbali za jirani na wanataraja kupata washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na mwenyeji Tanzania kushiriki mbio hizo baada ya kupata mrejesho kutoka kwao.

Mercy amesema mbio hizo za kilomita 21 na KM5 zitaaanzia barabara kuu na kuishia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kwa sasa kamati yao ipo katika maandalizi ya zawadi mbali mbali hasa uagizaji wa medali za kisasa sambamba na fedha taslim ambazo wataweka wazi baadae.

Kenya iliyokuwa kwenye karantini kwa sababu ya corona, tayari mipaka yao imefunguliwa na hilo limetoa fursa kwa wanariadha wao kuja kutetea kwa msimu wa tatu ubingwa wao.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz