Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya, Watanzania na Wasomali miongoni mwa washukiwa 35 wa ugaidi

Wakenya, Watanzania Na Wasomali Miongoni Mwa Washukiwa 35 Wa Ugaidi Wakenya, Watanzania na Wasomali miongoni mwa washukiwa 35 wa ugaidi

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Kenya imetoa majina na picha za washukiwa 35 wa ugaidi wanaoaminika kuhusika na mashambulizi ya hivi majuzi ya wanamgambo katika kaunti ya Lamu pwani.

Miongoni mwao ni Watanzania, Wasomali, Mjerumani, Mwingereza, Raia wa Bangladesh, huku wengi wao wakiwa Wakenya.

Washukiwa hao wanahusishwa na utegaji wa vilipuzi (IED) katika barabara mbalimbali na mauaji ya raia kwenye barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen.

Wanahusishwa pia na shambulio dhidi ya kambi ya jeshi la Marekani huko Manda Bay, Lamu, mnamo 2020.

Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema washukiwa hao "wenye silaha na hatari" walikuwa sehemu ya "mtandao wa kigaidi wa al-Shabab unaohusika na kupanga mashambulizi mabaya katika kaunti ya Lamu na msitu wa Boni ".

Mamlaka zinasema "zawadi kubwa" itatolewa kwa mtu yeyote aliye na habari kuhusu aliko mshukiwa yeyote.

Al-Shabab imeongeza mashambulizi katika mikoa ya kaskazini-mashariki na pwani ya Kenya katika miezi ya hivi karibuni.

Kundi la wanamgambo wenye mafungamano na al-Qaeda linakabiliwa na mashambulizi makubwa ya kijeshi nchini Somalia ambayo yanataka kuwatimua wanajihadi.

Chanzo: Bbc