Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya 21 wakamatwa na vyeti feki vya corona

Jkia T1 4 660x400 Wakenya 21 wakamatwa na vyeti feki vya corona

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Maafisa wa uwanja wa ndege nchini Kenya wamewakamata wasafiri 21 ambao waliokuwa wakielekea Dubai, katika Muungano wa Falme za kiarabu (UAE), kwa kutumia vyeti gushi vya Covid-19.

Wasafiri waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Wasafiri hao wamekamatwa wakati wa msako wa vyeti hivyo uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika Mji Mkuu, Nairobi.

Hii inakuja saa kadhaa baada ya UAE kupiga marufuku utoaji wa vibali vya kusafiria (visa) kwa wasafiri wanaotoka nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya.

Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa marufuku hiyo iliwekwa baada ya wasafiri kutoka Kenya kupatikana na vyeti gushi vya Covid-19 walipowasili katika taifa hilo la Ghuba.

Kenya imekuwa ikirekodi ongezeko la maambukizi ya Covid-19, huku jumla ya watu wenye maambukizi ikifikia 80,102 vikiwemo vifo vya watu 1,427.

NABII BUSHIRI, UTAJIRI WA KUTISHA, MALI KUSHIKILIWA, ANA NDEGE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI

Chanzo: millardayo.com