Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wake wa marais wa Burundi na Rwanda wakutana

Wake Wa Marais Wa Burundi Na Rwanda Wakutana Wake wa marais wa Burundi na Rwanda wakutana

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Kwa mara ya kwanza kama Mke wa Rais wa Burundi, Angeline Ndayishimiye ameizulu Rwanda kuhudhuria mkutano wa Women Deliver 2023 ambao umemkutanisha na mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.

Wake hawa wa marais wa Rwanda na Burundi wamekutana wakati nchi hizo mbili kwa sasa zikiimarisha uhusiano wao baada ya miaka mingi ya migogoro ya kisiasa na shutuma za mara kwa mara za pande mbili za kuingiliana kwa kijeshi.

Hata hivyo mara hii wanawake hawa wawili walikutana kwa ajili ya maendeleo ya wanawake, wasichana na vijana ambapo wanaendesha mashirika yanayohusika na maendeleo hayo la Jeannette Kagame Imbuto Foundation na Angeline Ndayizeye Bonne Action Charitable Foundation la Bi Angeline Ndayizeye.

Kando ya mkutano huu, Bi Ndayishimiye Ndayubaha alipokelewa na mwenzake wa Rwanda Jeannette Kagame na pia walibadilishana zawadi.Ofisi ya mke wa rais wa Burundi inasema kwamba wawili hao "walijadili mada zezinazohusu maslahi ya pamoja".

Katika kongamano la Women Deliver 2023, linalojadili mapambano ya kufikia usawa kati ya wavulana na wasichana, Angeline Ndayisimiye alitoa hotuba kuhusu ulinzi wa haki za wanawake kwa kuzingatia mkataba unaojulikana kwa jina la Maputo Protocol ya 2003, unaozungumzia haki za wanawake. Mwanamke barani Afrika.

Mkutano huu wa Women Delivery 2023 unaohudhuriwa na watu elfu sita (6000) kutoka pande zote za dunia, ni wa kwanza kufanyika katika bara la Afrika.

Baada ya kikao cha Jana Jumanne jioni, Angeline Ndayişimiye alirejea mara moja nchini mwake, kulingana na ofisi yake.

Chanzo: Bbc