Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wakimbia makazi yao DRC mashariki kwa kuhofia waasi wa M23

Wakazi Wakimbia Makazi Yao DRC Mashariki Kwa Kuhofia Waasi Wa M23 Wakazi wakimbia makazi yao DRC mashariki kwa kuhofia waasi wa M23

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: VOA

Wasiwasi mkubwa umeshuhudiwa katika Mji wa Rutshururu huko Kivu kaskaskazini mashariki mwa Congo DRC kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo la karibu na Matebe.

Wasiwasi mkubwa umeshuhudiwa katika Mji wa Rutshururu huko Kivu kaskaskazini mashariki mwa Congo DRC kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo la karibu na Matebe.

Mkaazi wa Rangira eneo linalopatikana kilometa chache mashariki mwa Mji wa Rutshuru aliyehifadhi jina lake ameshuhudia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo FARDC.

Katika eneo lao la Rangira karibu na Kijiji cha Matebe ambako waasi wa M23 wameonekana na kulazimisha wakazi kukimbia makazi yao kuhofia usalama wao.

Wakazi wengine waliomba jeshi la serikali kuwajibika vilivyo ili warudi kwa mara nyingine kwenye vijiji vyao.

Waasi wamefika katika eneo hilo huku bado jeshi likiwa mbali kabisa kwenye mstari wa mbele wa mapigano eneo la Rwanguba na Busanza. Wakazi hao waliondoka eneo la Matebe kwa hofu ya kujeruhiwa wakati wa mapigano makali.

Msemaji wa jeshi la Congo Cilvin Ekenge alisema Taifa la Congo lipo hatarini kuvamiwa na waasi wanaosaidiwa na mataifa Jirani ya Congo katika eneo la Afrikamashariki na lazima vyombo vya habari pamoja na wakazi kulinda usalama wa taifa wakishirikiana na serikali kuepuka kutangaza habari mbaya kuhusu jeshi.

Jeshi bado linaendelea kukabiliana na waasi wa M23 wanaoomba mazungumzo na serikali huku serikali ikisema ni kundi la kigaidi ambalo linayumbisha usalama wa DRC katika msaada wa mataifa jirani na haiwezi kuzungumza nao.

Chanzo: VOA