Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wakimbia Waasi wakiusogelea mji wa Goma

GettyImages 1246042977 Wakazi wakimbia Waasi wa M23 wakiusogelea mji wa Goma

Sun, 2 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa mji wa Goma nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanza kukimbia wakati ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiwa wanaujongelea mji huo muhimu.

Afisa mmoja wa serikali amenukuliwa akisema kuwa waasi wa M23 wanaukaribia mji wa Kanyabayonga uliopo kwenye njia inayoelekea katika mji wa Goma.

Kwa mujibu wa taarifa, mapigano yametokea kwenye eneo la Masisi karibu na mji wa Sake uliopo umbali wa kilometa 20 kutoka Goma.

Majeshi la serikali ya Kongo yamejaribu kuwarudisha nyuma waasi hao wa M23 wanaosemekana kuwa wameuzingira mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live