Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakati umewadia kuelewa mapenzi ya jinsia moja- Kadinali wa Ghana

Wakati Umewadia Kuelewa Mapenzi Ya Jinsia Moja  Kadinali Wa Ghana Wakati umewadia kuelewa mapenzi ya jinsia moja- Kadinali wa Ghana

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapenzi ya jinsia moja hayapaswi kuwa kosa la jinai na watu wanastahili kusaidiwa kuelewa suala hilo vyema, kadinali mmoja mkuu kutoka Ghana ameambia BBC.

Maoni ya Kadinali Peter Turkson yanakuja wakati bunge linajadili mswada unaotoa adhabu kali kwa watu wa wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Maoni yake yanakinzana na maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Ghana, wanaosema mapenzi ya jinsia ni kitu cha "kuchukiza mno".

Mwezi uliopita, Papa Francis aliashiria kuwa tayari kuwabariki wapenzi wa jinsia moja. Hata hivyo aliongeza, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Mwezi Julai, wabunge wa Ghana waliunga mkono hatua kali ichukiliwe dhidi ya wapenzi wa jinsia moja katika mswada uliopendekezwa, ambao bado haujaidhinishwa bungeni. Ungepitishwa bungeni ungefanya wale wanaojitambulisha kama wapenzi wa jinsia moja kuadhibiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Watu wanaoendesha kampeni ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja pia wanakabiliwa na hatari ya kufungwa jela hadi miaka 10.

Mapenzi ya jinsia moja tayari ni kinyume cha sheria na hukumu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela.

Katika taarifa yao mwezi Agosti, iliyotolewa pamoja na makukundi mengine makuu ya Kikristo nchini humo, maaskofu wa Ghana pia walisema kwamba nchi za Magharibi zinapaswa "kuzuia majaribio yasiyokoma ya kutuwekea maadili ya kitamaduni ya kigeni yasiyokubalika", gazeti la Catholic Herald liliripoti.

Kardinali Turkson, ambaye wakati fulani amekuwa akionekana kuwa mgombea wa baadaye wa papa, aliambia kipindi cha HARDtalk cha BBC kwamba "watu wa LGBT wanaweza wasihukumiwe kwa sababu hawajafanya uhalifu wowote".

"Ni wakati wa kuanza elimu, kusaidia watu kuelewa ukweli huu ni nini, jambo hili nini. Tunahitaji elimu zaidi ili kuwafanya watu ... kutofautisha kati ya uhalifu na sio uhalifu," aliendelea kusema.

Kadinali alisisitiza hoja hiyo akitolea mfano moja ya lugha za Ghana, Akan, kuna usemi "wanaume wanaofanya kama wanawake na wanawake wanaofanya kama wanaume".

Alidai kuwa hii ni dalili kwamba mapenzi ya jinsia moja sio mwenendo wa tabia kutoka nje. "Kama kiutamaduni tungekuwa na misemo... ina maana tu kwamba si geni kabisa kwa jamii ya Ghana."

Hata hivyo, Kadinali Turkson alisema anafikiri kwamba kilichosababisha juhudi za sasa za kupitisha hatua kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja katika nchi kadhaa za Afrika ni "majaribio ya kuunganisha baadhi ya michango na misaada ya kigeni na maslahi fulani ... kwa nia ya kupigania uhuru, kutetea haki".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live