Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa 'Airport' wakiwa wameficha heroine kwenye chakula cha watoto

Heroine Niger Niger Wakamatwa 'Airport' wakiwa wameficha heroine kwenye chakula cha watoto

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dawa za kulevya aina ya heroine zilizofichwa ndani ya pakiti za vyakula vya watoto imenaswa katika uwanja wa ndege mkuu wa Lagos, kwa mujibu wa polisi.

Washukiwa watatu wamekamatwa kuhusiana na kusafirisha kilo 23 za dawa hiyo kwenye Shirika la Ndege la Afrika Kusini kutoka Johannesburg, alisema msemaji wa Shirika la Kitaifa la Kupambana na Dawa za Kulevya Femi Babafemi siku ya Jumapili.

Katika tukio tofauti, shirika la kupambana na dawa za kulevya lilisema dereva wa usafiri wa umma alikamatwa katika uwanja huo huo wa ndege kwa tuhuma za "kumeza kete 90 za cocaine" kabla ya kujaribu kupanda ndege kuelekea Dubai.

Maafisa nchini Nigeria mara nyingi wameelezea kuenea kwa matumizi ya dawa za kulevya nchini humo kuwa ni jambo la kutisha na janga.

Pia ni sehemu ya kupitisha dawa mbalimbali haramu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live