Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajumbe wa SADC kutatua mgogoro Eswatini

Eswatin Pic Afrika Kusini imetuma wajumbe wa SADC kutatua mgogoro falme za Eswatini

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametuma timu kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kwenda kwenye falme za Eswatini kutatua mgogoro unaoendelea licha ya kusema mara kadhaa kuwa amechoka kutatua migogoro isiyoisha katika falme hiyo.

Kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, Siasa na Ushirikiano wa SADC, Ramaphosa aliteua wajumbe watatu kutoka Afrika Kusini kuzungumza na mfalme Mswati wa tatu wa falme hiyo.

Timu hiyo inakusudiwa kwenda kujadili mzozo wa kisiasa kati ya Mfalme huyo na watendaji walioteuliwa kuendelea kufanya kazi kwenye utawala wake, jambo ambalo limeibua mgogoro mkubwa na kusababisha maandamano makubwa ya raia.

Inadaiwa kuwa Jeshi la Polisi limeripotiwa kuhusika na mashambulizi ya moja kwa moja kwa raia yaliyojeruhi raia 20 huku wengi wakiwa hawajulikani walipo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live