Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajackoyah amtaka Ruto kuruhusu askari wanawake kuvaa hijabu

Hijabu Askari Madc Wajackoyah amtaka Ruto kuruhusu askari wanawake kuvaa hijabu

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022 Profesa George Wajackoyah ametoa wito kwa Rais William Ruto kuhusu sare za wanawake wa dini ya Kiislamu ambao ni maafisa wa polisi.

Wajackoyah sasa anamtaka Rais Ruto akuwaruhusu maafisa hao wa polisi kuvaa hijab chini ya kofia zao ili kuendana na imani yao ya Kiislamu hata wakiwa kazini.

"Ninataka wanawake wa Kiislamu ambao ni maafisa wa polisi waruhusiwe kufunika vichwa vyao kutumia hijab. Kofia ya polisi iwe juu ya hijab. Ninataka Waislamu kuwakilihwa kila mahali," Wajackoyah alisema akiwa Mumias mnamo Jumatatu - Januari 16.

Kiongozi huyo wa chama cha Roots pia aliitaka serikali kuwatengea likizo ya kila wiki waumini wa dini ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Wajackoyah, waumini wa dini zingine wana likizo kwa ajili ya siku zao za ibada na kupumzika huku Waislamu wakiwa hawana siku yoyote ile.

"Ninataka serikali kutenga Ijumaa kuwa likizo kwa Waislamu. Wanasabato wana Jumamosi na Wakristo wana Jumapili lakini Waislamu hawana siku yao," Wajackoyah amesema.

Katika kampeni zake, Wajackoyah aliahidi Wakenya kuwa na siku tatu za likizo kila wiki angekuwa rais wa tano wa Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live