Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajackoyah adai atashinda urais Kenya

Wajakhoha Data Wajackoyah adai atashinda urais Kenya

Sun, 14 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Chama cha Roots ambacho kilimsimamisha Profesa George Wajackoyah kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kenya, uliofanyika Agosti 9, 2022 kimesema kina imani mgombea wao atashinda kiti hicho kupitia mchakato huru na wenye usawa wa kumpata mshindi.

Wajackoyah hadi leo saa 12:12 jioni Jumapili Agosti 14, 2022 alikuwa na kura 59,461 ambazo ni sawa na asilimia 0.44 akiachwa mbali na mgombea wa Kenya Kwanza, William Ruto anayeongoza kwa kupata kura milioni 6.7, Raila Odinga anayefuatiwa kwa kura milioni 6.6.

Kauli hiyo, imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Adam Kadernani kupitia taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari huku ikiungwa mkono na mgombea wa chama hicho, George Wajackoyah aliyeiweka kwenye mtandao wake wa twitter.

“Tuna uhakika kuwa tutashinda kupitia mchakato wenye usawa, uhuru na haki kwenye kumpata mshindi wa nafasi hiyo,”taarifa hiyo imesema.

Kwenye taarifa hiyo pia, imeonyesha kuwa Wajackoyah amewataka Wakenya wote kutunza amani na kuwa wavumilivu kipindi ambacho Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya inahakiki matokeo ya urais.

Chama cha Roots kimetoa taarifa hiyo muda mfupi tangu mgombea wa urais wa Chama cha Agano, David Waihiga akubali kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Chanzo: Mwananchi