Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu wa Nigeria waunga mkono Palaestina

Waislamu Nigeria Waislamu wa Nigeria waunga mkono Palaestina

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waislamu nchini Nigeria wameandamana na kusisitiza uungaji mkono wao mkubwa kwa wananchi wa Palestina na muqawama wao dhidi ya uvamizi wa Israel na jinai zao.

Waislamu katika Jimbo la Bauchi la Nigeria walifanya maandamano wakipeperusha bendera za Palestina huku wakitoa nara za "Tunaunga mkono Hamas," "Tunaunga mkono Palestina," "Mauti kwa Israel na Mauti kkwa Marekani".

Katika hotuba yake kwenye mkusanyiko wa waandamanaji hao, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika eneo la Kaskazini Mashariki la Bauchi, Sheikh Ahmad Yusuf Yashi amesema "Israel iliapa kuwaangamiza Wapalestina na kuwanyang'anya ardhi yao yote. Hivi ninavyozungumza nanyi sasa, utawala wa Kizayuni unashambulia kwa mabomu Gaza, na kuua wanawake na watoto wasio na hatia baada ya Harakati ya Muqawama ya Hamas kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya vikosi vya Kizayuni.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake wa haki ambao unaifanya Palestina iendelee kuwepo licha ya miongo kadhaa ya ugaidi wa Israel.

Katika Jimbo la Kano, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, wafuasi wa Palestina waliingia barabarani kuupongeza muqawama wa kishujaa wa Wapalestina walioidhalilisha Israel.

Sheikh Sunusi Abdulqadir, mwakilishi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky alionekana akiwagawia watu masikini chakula kuonesha furaha yao kuhusu mafanikio ya Wapalestina kutokana na kulipiza kisasi dhidi ya utawaala ghaasibu wa Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live