Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waislamu Nigeria waandamana na kulaani uchochezi wa jarida la Kifaransa

Waislamu Maandamano.jpeg Waislamu Nigeria waandamana na kulaani uchochezi wa jarida la Kifaransa

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: Mwananchi

Waislamu nchini Nigeria wameandamana tena na kulaani kitendo cha dharau, kejeli na udhalilishaji cha jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo cha kuchapisha vibonzo vya kumvunjia heshima Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara dhidi ya kuvunjiwa heshima viongozi wa dini na kulaani vikali hatua ya serikali ya Ufaransa ya kulikingia kifua gazeti hilo ambalo huko nyuma pia liimewahi kuchapisha vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).

Sheikh Sanusi Abdulkadir mmoja wa viongozi wa Kiislamu nchini Nigeria amesema mbele ya mkusanyiko wa waandamanaji hao kwamba, Waislamuu katu hawakubaliani na suala la kuvukwa mistari yao myekundu.

Aiidha waandamanaji hao walisikika wakika wakipiga nara za "Allah Akbar" na Labbayka ya Rasullah" na kusisitiza kwamba, katu hawawezi kustahamili kitendo cha Wafaransa cha kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

Katika toleo lake maalumu la tarehe 4 mwezi huu (Januari) jarida hilo la Ufaransa lilifanya kitendo cha kipuuzi cha kuanzisha shindano la kimataifa la michoro na vibonzo, ambapo lilichapisha picha za kuudhi zilizoandamana na maneno na misemo michafu na ya matusi dhidi ya Kiongozi Muadhamu.

Kufuatia hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kukashifu na kuvunjia heshima wanazuoni, matukufu na thamani za kidini na kitaifa za Iran, balozi wa Ufaransa mjini Tehran aliitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ili kubainishiwa malalamiko ya Iran kuhusu kitendo hicho cha dharau.

Chanzo: Mwananchi