Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waingereza waliokolewa Gaza wana saa 72 kuondoka Misri

Waingereza Waliokolewa Gaza Wana Saa 72 Kuondoka Misri Waingereza waliokolewa Gaza wana saa 72 kuondoka Misri

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Watu wa Uingereza na raia wengine wa kigeni ambao wameokolewa Gaza wana saa 72 pekee - siku tatu - nchini Misri kabla ya kuhitajika kuondoka.

Mamia ya raia wa kigeni walihamishwa kutoka Gaza hadi Misri kupitia kivuko cha Rafah siku ya Ijumaa.

Mpaka ulifungwa wikendi yote.

Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) ilisema: "Tunasalia kuwasiliana na raia wa Uingereza katika eneo hili ili kuwapa taarifa za hivi punde."

Iliongeza katika taarifa yake kuwa "inatumia njia zote za kidiplomasia kushinikiza kuvuka kufunguliwe tena kwa uratibu na washirika wetu wa kimataifa".

Nasser Alshanti, msomi kutoka Manchester, aliambia BBC kwamba binti yake mjamzito Yosra "amekwama" nchini Misri kwa sababu mumewe si raia wa Uingereza, na wana wasiwasi kwamba hawataweza kuondoka ndani ya siku tatu zilizowekwa.

Yosra alilelewa nchini Uingereza na kuhamia Gaza kujiunga na chuo kikuu mwaka 2015, ambako alikutana na mchumba wake - na kisha akaolewa na Ibrahim. Wanandoa hao walikuwa wakiishi katikati mwa Gaza tangu wakati huo, hadi walipolazimika kutoroka katika wiki ya kwanza ya vita wakati kitongoji chao kililipuliwa kwa bomu.

Walihamishwa kutoka Gaza hadi Misri kupitia kivuko cha mpaka cha kusini huko Rafah mwishoni mwa wiki iliyopita, na sasa wako Cairo.

Kwa sababu Ibrahim si raia wa Uingereza, sasa wanahitaji kumwombea Visa ya Familia kabla ya kusafiri hadi Uingereza.

Lakini makataa ya saa 72 nchini Misri yanamaanisha kuwa wana wasiwasi kuhusu kukaa zaidi ikiwa hawatapata visa kwa wakati.

Chini ya sheria za sasa, kukaa zaidi kunaweza kumaanisha kulipa faini, ambayo inaweza kuwa kubwa zaidi kadiri wanavyoendelea kukaa.

Chanzo: Bbc