Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waiba gari la polisi na kutokomea nalo

Gari Ya Polisi Kenya Wizi Waiba gari la polisi na kutokomea nalo

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: Mwananchi

Katika tukio lisilokuwa la kawaida watu wanne wamedaiwa kuliiba gari ya Polisi kisha kutokomea nayo kusikojulikana nchini Kenya.

Inaelezwa watu hao walimvizia askari aliyekuwa na gari hiyo alipokuwa kituo cha mafuta kisha kumnyang’anya kwa nguvu.

Tovuti ya Tuko ya nchini humo imesema tukio hilo limetokea juzi Jumamosi alfajiri ya Desemba 23, 2023 mkabala na barabara ya Kisumu.

Taarifa zaidi zinasema mmoja ya watu hao alikuwa na bunduki aina ya AK47 ambapo askari huyo anayefanya kazi katika kituo cha polisi cha Nyamasaria walimuibia pia na vitu vyake vingine.

“Kulingana na uchunguzi, mmoja wa watu hao alimwendea askari aliyekuwa na gari hiyo kabla ya wenzake watatu kujitokeza. Walimzidi nguvu na kumtoa kwenye gari na kumjeruhi kwenye mguu wake wa kulia.

“Kisha walitokomea na gari hilo. Aidha waliiba begi, redio ya polisi, daftari la polisi, pochi iliyokuwa na kadi ya ATM, kitambulisho, kadi ya bima ya afya na cheti cha kuteuliwa cha polisi,” imeeleza tovuti hiyo.

Chanzo: Mwananchi