Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahariri wataka uchunguzi mauaji ya mwandishi wa habari

Arshad Sharif  .jpeg Wahariri wataka uchunguzi mauaji ya mwandishi wa habari

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Wahariri nchini Kenya (KEG) kimetoa wito ufanyike uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji ya kushtua ya mwanahabari wa Pakistani, Arshad Sharif.

Sharif aliuawa na polisi huko Kajiado nchini Kenya juzi Jumapili usiku baada ya kudhaniwa kuwa ni mwizi aliyedaiwa kuiba gari katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa jana tarehe 24 Oktoba, 2022 na Rais wa KEG, Churchill Otieno ametaka uchunguzi wa kina ufanywe kubaini ni kwa nini mwanahabari huyo mashuhuri aliuawa, pamoja na kukamatwa kwa waliohusika.

Pia alisema uchunguzi wa kina utadhihirisha uwezo wa uchunguzi wa vyombo vya dola vya nchi hiyo na kuwahakikishia Wakenya na raia wa kimataifa usalama wa nchi.

“Tunaposubiri maelezo yote kuhusu mauaji hayo, Chama cha Wahariri wa Kenya kinaitaka Serikali kuchunguza kwa haraka na kwa kina kisa hicho ili kubaini chanzo na sababu ya mauaji hayo na kuwafikisha waliohusika mahakamani,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

“Hii haitaonyesha tu uwezo wa Kenya na serikali wa kulinda raia na wageni wake lakini pia kuwahakikishia Wakenya na jumuiya ya kimataifa kwamba Kenya ni salama kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na wanahabari ambao inapaswa kulinda haki zao.” Pia KEG ilituma risala za rambirambi kwa familia ya mwanahabari huyo.

Arshad Sharif alipigwa risasi kichwani na kuuawa na polisi baada ya yeye na dereva wake kudaiwa kukiuka kizuizi cha barabarani kilichokuwa kimewekwa kuangalia magari yanayotumia njia hiyo.

“Walikuwa wakiendesha gari kutoka mji wa Magadi kuelekea Nairobi walipotakiwa kusimama kwenye kizuizi cha barabarani kilichokuwa na kundi la maafisa wa polisi,” polisi walisema.

Kulingana na polisi, katika kizuizi hicho cha barabarani, kulikuwa na mwito kwa polisi kulizuia gari sawa na walilokuwa wakiendesha kufuatia tukio la utekaji nyara eneo la Pangani, Nairobi ambapo mtoto alitekwa nyara.

Dakika chache baadaye, gari la Sharif lilijitokeza kwenye kizuizi cha barabara na wakasimamishwa na kutakiwa kujitambulisha. Inadaiwa walishindwa kusimama na kupita kwenye kizuizi cha barabarani.

Hii ilisababisha kufukuza na kupigwa risasi kwa muda mfupi na kumwacha Sharif. Gari lao lilibingirika na dereva wake alijeruhiwa na kupelekwa hospitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live