Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji zaidi ya 20 wafariki ajali ya boti Senegal

Boti Ya Wahamiaji Yazama Na Kuua Watu Sita Pwani Ya Ufaransa Wahamiaji zaidi ya 20 wafariki ajali ya boti Senegal

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya miili 20 iliopolewa baharini kaskazini mwa Senegal siku ya Jumatano baada ya kuzama kwa boti ya wahamiaji iliyokuwa ikielekea Ulayakulingana na shuhuda, gavana wa eneo la Saint-Louis ameliambia shirika la habari la AFP.

"Zaidi ya miili 20" ilipatikana, amesema Alioune Badara Samb, aliyehojiwa kwa simu. Takriban watu ishirini waliokolewa, ameongeza.

Hakuzungumzia idadi ya abiria waliokuwa kwenye boti hapo awali. Lakini shuhuda kutoka kwa walionusurika zilizokusanywa na mwandishi wa shirika la habari la AFP zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu walikuwa ndani ya boti na kwa hivyo hawakupatikana.

Mamady Dianfo, mwenye asili ya Casamance (kusini ), amesema zaidi ya abiria 300 ambao walikuwa nadani ya boti hiyo wakati ilipoondoka kwenye pwani ya Senegal wiki moja iliyopita. Mtu mwingine aliyenusurika, Alpha Baldé, amesema abiria walikuwa zaidi ya 200.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live