Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji waliokwama Tunisia watajwa kuwa na hali mbaya

Watetea Haki Za Binadamu Waomba Msaada Wahamiaji 360 Wahamiaji waliokwama Tunisia watajwa kuwa na hali mbaya

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mamia ya wahamiaji haramu wa nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara waliokwama kwenye mpaka kati ya Libya na Tunisia wanaishi katika hali mbaya baada ya kufukuzwa na serikali ya Tunisia.

Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa doria za jangwani za Idara ya Kudhibiti Uhamiaji Haramu nchini Libya, Bw. Abdulla al Fak'hal.

Amesema: "Idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la Sahara wamekwama katika eneo kubwa la jangwani kati ya Tunisia na Libya. Wanaishi katika hali mbaya mno, bila ya chakula wala maji ya kunywa tena katika hali ya joto kali.

Mgogoro wa kibinadamu katika mpaka wa Tunisia na Libya umeongezeka vibaya katika kipindi cha wiki za hivi karibuni. Watu wengi wanateketea na kupoteza maisha kutokana na joto kali, kiu na njaa kali. Miili zaidi ya wahamiaji imegunduliwa na Kikosi cha Udhibiti wa Mipaka cha Libya katika maeneo yasiyokaliwa na watu kwenye wiki za hivi karibuni. Tamaa mbele mauti nyuma. Wakimbizi wengi wanahatarisha maisha katika safari hatari za mauti za kujaribu kufika barani Ulaya kwa tamaa ya eti kupata maisha bora.

Hali ya wakimbizi na wahamiaji haramu nchini Libya ni mbaya kiasi kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo hiri karibuni alitoa mwito wa kuungwa mkono kimataifa Libya katika suala la uhamiaji haramu.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdul Hamid al-Dbeibeh alisema wiki iliyopita kwamba: Jamii ya kimataifa inapaswa kutoa msaada wa kisiasa, kimaada na kiusalama kwa Libya katika suala la wahajiri haramu.

Maelfu ya wahajirii na wakimbizi wamekuwa wakiaga dunia kila mwaka katika Bahari ya Mediterania na majangwa kwa tamaa ya kufika Ulaya.

Nchi za kaskazini mwa Afrika kama Libya na Tunia zinatumiwa sana na wahajiri hao katika safari za hatari na mauti ya kujaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya.

Chanzo: mwanachidigital