Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji walioachwa mpaka wa Tunisia na Libya wameondolewa

Wahamiaji Walioachwa Mpaka Wa Tunisia Na Libya Wameondolewa Wahamiaji walioachwa mpaka wa Tunisia na Libya wameondolewa

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: Voa

Wahamiaji wote 500 hadi 700 waliokuwa kwenye mpaka wa Libya wamehamishiwa kwingineko, Salsabil Chellali wa shirika la Human Rights Watch (HRW) mjini Tunis ameliambia shirika la habari la AFP

Mamia ya wahamiaji walioachwa wakiwa wamekwama katika mazingira magumu katika mpaka wa Tunisia na Libya baada ya kukimbia ghasia, waliondolewa siku ya Jumatatu, shirika lisilo la kiserikali limesema lakini hofu imebakia kwa dazeni wengine waliolazimishwa kuelekea Algeria.

Mivutano ya ubaguzi wa rangi ilizuka katika ghasia dhidi ya wahamiaji kutoka nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara katika mji wa bandari wa Sfax nchini Tunisia wiki iliyopita, huku mamia wakikimbia au kusukumwa katika maeneo yasiyo salama katika mpaka wa kusini mwa jangwa la Sahara.

Wahamiaji wote 500 hadi 700 waliokuwa kwenye mpaka wa Libya wamehamishiwa kwingineko, Salsabil Chellali wa shirika la Human Rights Watch (HRW) mjini Tunis ameliambia shirika la habari la AFP.

Lakini watu wengine wengi waliofukuzwa karibu na mpaka wa Algeria wanahatarisha maisha yao ikiwa hawataokolewa mara moja, alieleza. HRW inakadiria idadi ya watu hao kuwa 150 hadi 200.

Chanzo: Voa