Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji kutoka Afrika waongezeka Mexico

Wahamiaji Mexico (600 X 321) Wahamiaji kutoka Afrika waongezeka Mexico

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya wahamiaji kutoka Afrika waliowasili Mexico mwaka jana imeongezeka mara tisa zaidi ya mwaka wa nyuma yake.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Mambo ya Ndani ya Mexico zimeonesha kwamba wahamiaji 60,000 kutoka Afrika waliwasili nchini humo mwaka jana 2023, wakati mwaka wa nyuma yake Mexico ilipokea wahamiaji 6,500 kutoka Afrika. Takwimu za mwaka huu bado zinakusanywa.

Dana Graber Ladek, mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na wahamiaji nchini Mexico, limeiambia BBC kwamba wengi wa wahamiaji hao wanatoka nchi za Guinea, Angola, Mauritania, Senegal, Nigeria na Cameroon.

Amesema: "Watu hao huondoka katika nchi zao kwa sababu kadha wa kadha kuanzia machafuko ya kisiasa hadi umaskini uliokithiri. Lakini pia amesema kuna sababu zinazotokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na majanga ya asili."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live