Walinzi wa pwani za Tunisia wamepata miili 58 ya wahamiaji na wameokoa wahamiaji wengine 1,242 katika muda wa saa 48 zilizopita nje ya pwani za nchi hiyo.
Hayo yamo kwenye taarifa ya jana Jumanne ya Walinzi wa Taifa wa Tunisia ambao wamesema, kundi la watu walionusurika linajumuisha 1,207 kutoka nchi za Afrika za kusini mwa Jangwa la Sahara, na wengine kutoka nchini Tunisia na nchi zingine za Kiarabu.
Msemaji wa Gadi ya Taifa ya Tuniam Houcemeddine Jbabli amesema hayo kwenye taarifa yake na kuongeza kwamba, wahamiaji hao walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuelekea kisiwa cha Lampedusa cha chini Italia.
Haya yanajiri baada ya walinzi wa pwani za Tunia kupata miili 31 ya wahamiaji wasio na vibali katika fukwe za majimbo ya Sfax, Mahdia na Gabes Jumamosi jioni.
Wakati wa msimu wa masika na kiangazi, idadi ya wahamiaji wanaopigania kufika kwenye fukwe za Italia kupitia pwani ya Tunisia huongezeka sana kutokana na hali nzuri ya hewa.
Tunisia ni moja ya maeneo maarufu ya nayopenda na waamiaji haramu wanaoelekea barani Ulaya kutokana na kuwa kwake kwenye eneo zuri la Bahari ya Mediterania na karibu na bara Ulaya.