Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahalifu wa kimtandao waingilia kompyuta za uhamiaji Malawi

Malawi Yasitisha Safari Zote Za Serikali Za Nje Ya Nchi Wahalifu wa kimtandao waingilia kompyuta za uhamiaji Malawi

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Malawi imesitisha utoaji wa hati za kusafiria kufuatia uhalifu wa kimtandao uliofanywa kwenye kompyuta za huduma za Idara ya Uhamiaji.

Rais Lazarus Chakwera amewaambia wabunge kwamba kulengwa kwa idara hiyo na wahalifu ni sawa na "ukiukaji mkubwa wa usalama wa taifa".

Amefichua kuwa wadukuzi hao wa siri za Uhamiaji walikuwa wakiomba fidia ili warejeshe mambo katika ukawaida wake.

Lakini rais amesema serikali haitakubali madai yao na kwamba inapambana kutatua tatizo hilo na kuwakamata.

"Hatuko katika biashara ya kuwaridhisha wahalifu kwa pesa za umma, wala hatuko katika biashara ya kufanya mazungumzo na wale wanaoshambulia nchi yetu," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live