Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa 3 waaga dunia Nakuru baada ya kiwanda cha oksijeni kupata hitilafu

97cbcb538bae6730 Wagonjwa 3 waaga dunia Nakuru baada ya kiwanda cha oksijeni kupata hitilafu

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kiwanda hicho kilichoko katika hospitali ya Nakuru Level Five kiliharibika mwishoni mwa juma na kusababisha uzalishaji mdogo wa oksijeni

- Afisa wa Afya kaunti hiyo Gichuki Kariuki alisema kiwanda hicho kilishindwa kuzalisha mitungi 80 inayohitajika

- Wagonjwa watatu waliokuwa wakiongezewa hewa walipoteza maisha yao wakati wa kisa hicho cha kusikitisha

Serikali ya kaunti ya Nakuru imethibitisha vifo vya wagonjwa watatu wa COVID-19 baada ya kiwanda cha kuzalisha oksijeni kupata hitilafu mwishoni mwa juma.

Kiwanda hicho kilichoko katika hospitali ya Nakuru Level Five kiliharibika Jumamosi, Aprili 10, na kusababisha uzalishaji mdogo wa oksijeni kukidhi mahitaji ya idadi ya wagonjwa waliohitaji hewa.

Afisa wa Afya kaunti hiyo Gichuki Kariuki alisema kiwanda hicho kilishindwa kuzalisha mitungi 80 inayohitajika na badala yake kuzalisha 40.

Wagonjwa hao watatu walikuwa wakiongezewa hewa wakati wa tukio hilo la kisikitisha

Afisa mkuu mtendaji wa Hewa Tele Zulfiqar Wali ambaye anamiliki kiwanda hicho alithibitisha kuwa walisitisha uzalishaji wa oksijeni kwa karibu saa nane wakati wahandisi wakifanya ukarabati.

"Kwa saa nane mfululizo, tuliacha shughuli zetu za kawaida ili kujituma kushughulikia mashine iliyopata hitilafu. Tunafurahi kwamba wahandisi wetu waliweza kukarabati mfumo wa kiwanda haraka iwezekanavyo," alisema.

Mnamo Jumanne, Aprili 13 Wizara ya afya ilitangaza kwamba watu wengine 26 walipoteza maisha yao kutokana na makali ya virusi vya corona.

Idadi sasa ya waliofariki dunia imetimia 2,394.

Wizara hiyo aidha ilitangaza wagonjwa 239 wamo kwenye ICU nao 47 wamewekwa kwenye ventileta.

Wagonjwa wengine 293 wanaongezewa oksijeni.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke