Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea Urais Congo waikalia kooni mahakama

Dr Congo Flag Wagombea Urais Congo waikalia kooni mahakama

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagombea sita wa upinzani katika uchaguzi wa Rais wa Disemba 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana waliiomba Mahakama ya katiba ya nchi hiyo kuilazimisha tume ya uchaguzi kuchapisha orodha ya mwisho ya wapigakura, wakionya juu ya uwezekano wa kukikwa ksheria na kujiri udanganyifu.

Wagombea hao ni pamoja na mpinzani mkuu Martin Fayulu mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Fayulu ambaye anagombea kiti cha urais huko Kongo amedai kuwa kuna makosa ya kimakusudi yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo yanatilia shaka kutumiwa daftari la wapiga kura. Martin Fayulu

Msemaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amekataa kutoa maelezo kuhusu tuhuma hizo dhidi ya tume hiyo. Awali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Kongo alipinga tuhuma kama hizo zilizotolewa na upande wa upinzani. Alisema katika mkutano na waandishi wa habari mwezi Oktoba mwaka huu kuwa tume hiyo itahakikisha uchaguzi wa Disemba utakuwa huru na wa haki.

Wagombea hao sita wa kiti cha urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walisema jana katika taarifa yao ya pamoja kuwa kuchapisha orodha ya wapigakura kama ilivyoainishwa na sheria kutaruhusu muda wa kutosha kurekebisha masuala yote yenye shaka na kuwawezesha wapiga kura kujua ni wapi watapiga kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live