Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea 2,350 kuwania viti 113

Togoooo Wagombea 2,350 kuwania viti 113

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Kikatiba nchini Togo imeidhinisha wagombea 2,350 kati ya viti 113 vinavyogombaniwa katika nafasi ya ubunge nchini humo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Aprilli 20, 2024.

Katika orodha hiyo vimo vyama kumi na tisa vya kisiasa ambavyo vitaingia katika uwanja wa kisiasa kupata wawakilishi katika bunge lijalo.

Hata hivyo Chama cha Alliance ensemble kimelaani muda uliochukuliwa na Mahakama ya Kikatiba wa kuweka orodha hizo hadharani kikielezea Mahakama kutozingatia ratiba na kuwepo kwa makosa katika majina yaliyoorodheshwa.

Kwa upande wa Paul Dodzi ameonyesha wasi wasi wake kuhusiana na upigaji kura ambao unaweza kuwa mgumu kwa raia wa nchi hiyo kutokana na wingi wa wagombea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live