Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wageni waendelea kumiminika mtaani Karen kukutana na DP Ruto

44cdd57aa9649069 Wageni waendelea kumiminika mtaani Karen kukutana na DP Ruto

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Karen kumegeuka na kuwa uwanja wa kupanga siasa za DP kuingia Ikulu ifikapo 2022Amekuwa akikutana na wafuasi wake ambao huwauzia injili yake ili wasaidie kuisambaza mashinaniDP na wandani wake wanaamini hakuna kitu au mtu anaweza kuwa kizuizi katika safari yake ya kuingia IkuluNaibu Rais William Ruto anaendelea kuwapokea wageni nyumbani kwake mtaani Karen ambapo wadadisi wanasema kumegeuka uwanja wa kucheza siasa zake.

Baada ya serikali kufunga shughuli zote za kisiasa kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya Covid-19, DP aligeuza Karen kuwa eneo la kukutana na wafuasi wake.

Alhamisi Juni 24 hilo liliendelea ambapo alikutana na viongozi kutoka kaunti ya Tharaka Nithi wakiongozwa na wabunge Beatrice Nkatha na Patrick Munene.

Ruto alisema mazungumzo yake na viongozi hao, ambao walijumuisha MCAs, ilikuwa kuwataka waendelee kuwa macho ya wananchini bungeni.



Awali DP alikuwa amefanya kikao kingine na kundi la vijana kutoka Nairobi, Mt Kenya na Lamu na kuwataka kushiriki mjadala kuhusu uchumi wa Kenya.

Ruto alisema vijana wanafaa kuwa katika mstari wa mbele wakati huu ambapo kuna mdahalo kuhusu mfumo wa kiuchumi unaofaa kuangaziwa.

"Tunawataka vijana kushiriki mjadala wa kitaifa kuhusu njia za kufufua uchumi wa taifa kwa sababu kufanya hivyo ni kuwa wazalendo," alisema DP.



DP Ruto ameweka wazi ndoto yake ya kuingia IKulu na ksuema hakuna kitu au mtu anaweza kuwa kizuizi kwake.

Amekuwa akipanga mikakati yake kwa kuwahusisha viongozi wa mashinani ambao huwabatiza na kuwa washirika wa kueneza injili yake.

Matunda ya juhudi zake yamekuwa yakionekana huku viongozi kama vile Gathoni Wamuchomba wakihama Kieleweke na kujiunga na kambi yake ya Tangatanga.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke