Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waganda wakasirishwa serikali kuipa barabara jina la watalii waliouawa

Waganda Wakasirishwa Serikali Kuipa Barabara Jina La Watalii Waliouawa Waganda wakasirishwa serikali kuipa barabara jina la watalii waliouawa

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Uamuzi wa serikali ya Uganda kuipa barabara jina la watalii wawili wa kigeni waliouawa nchini humo mapema mwezi huu umeibua hasira.

Raia wa Uingereza David Barlow na mkewe wa Afrika Kusini Emmaretia Geyer waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa kwenye fungate yao.

Polisi walisema washambuliaji hao pia walichoma gari lao katika shambulio hilo la Oktoba 17.

Baadhi ya Waganda wameikosoa serikali kwa kuwaheshimu wanandoa hao wa kigeni lakini bila kujumuisha Eric Alyai, raia wa Uganda aliyeuawa pamoja nao.

Mamlaka zinasema wanandoa hao, kutoka Berkshire nchini Uingereza, walikuwa kwenye ziara ya kuwaona sokwe katika Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth walipouawa katika shambulio la Allied Democratic Forces (ADF).

ADF ni kundi la waasi lenye uhusiano na Dola la Kiislamu ambalo linapatikana magharibi mwa Uganda, lakini linaendesha shughuli zake katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

"Kama baraza la mawaziri, tumefikia uamuzi kwamba kwa watalii hawa, tutaita moja ya barabara nchini Uganda kwa heshima yao," waziri wa wa Mawasiliano wa Uganda Chris Baryomunsi alinukuliwa akisema na tovuti ya Uganda ya The Nile Post.

Hakutaja jina la barabara. Kuhusu Bw Alyai, Mganda aliyeuawa pamoja na watalii hao, alisema kwamba serikali ingesaidia familia yake.

Chanzo: Bbc